Home » Tanzania » Bw. Charles E. Kichere kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Bw. Charles E. Kichere kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

21 November 2016 | Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 20 Novemba, 2016 amemteua Bw. Charles E. Kichere kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Bw. Charles E. Kichere anajaza nafasi ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA iliyokuwa wazi kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Uteuzi huu umeanza mara moja.

 

 

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

20 Novemba, 2016

 

Ad