Home » Tanzania » Alphonse Charahani: Mhandisi wa MV Nyerere aokolewa akiwa hai siku tatu baadaye

Alphonse Charahani: Mhandisi wa MV Nyerere aokolewa akiwa hai siku tatu baadaye

23 September 2018 | Tanzania

Mhandisi wa kivuko cha MV Nyerere Alphonse Charahani ameokolewa leo alfajiri akiwa hai.

Kwa sasa Charahani anaendelea kupokea matibabu kutoka kituo cha afya cha Bwisya Ukara.

Kufikia sasa idadi ya miilio iliopatikana ni 211 huku zaidi ya milli 116 kati yao ikitambuliwa na ndugu zao kulingana na waziri wa uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe.

Kulingana na waogeleaji Charahani alidaiwa kujipaka mafuta miwilini ambayo wameelezea kusaidia maji kutoweza kuingia kupitia vinyweleo.

Shughuli za uokoaji zinatarajiwa kuendelea leo baada ya kusitishwa jana usiku kutokana na giza.

Kwa mujibu wa maafisa wa serikali mkoani humo, mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika huku nahodha wa meli hiyo akiwa miongoni mwa waliofariki dunia.

Mwandishi wa BBC David Nkya awali alizungumza na mkuu wa wilaya ya Ukerewe Kanali Lucas Maghembe ambaye anasema kufikia wakati wa kusitishwa kwa juhudi za uokoaji Alhamisi jioni, waokoaji walikuwa wamechunguza ndani ya kivuko hicho na hakukuwa na dalili za kuwapata manusura wakiwa hai.

Amesema uchunguzi unaendelea na iwapo kulikuwa na utepetevu fulani uliosababisha ajali hiyo wahusika watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Kanali Magembe amesema pia kwamba ikizingatiwa kwamba maeneo mengi eneo hilo ni maji, mfano Ukerewe ambapo maji ni asilimia 90, eneo hilo linahitaji meli na vyombo vingine vya usafiri ambavyo vipo katika hali nzuri.

Rais Magufuli aeleza kuwa miili ya watu takriban 131 imeopolewa

Haki miliki ya picha Reuters Image caption Rais John Pombe Magufuli aeleza kuwa miili ya watu takriban 131 imeokolewa

Rais John Magufuli amehutubia waandishi muda mfupi uliopita na ameeleza kuwa kufikia sasa imethibitika kwamba miili ya watu 131 imeokolewa na bado kuna hofu kwamba wengine wengi hawajapatikana.

Ameeleza kuwa rasmi kivuko hicho cha MV Nyerere kina uwezo wa kubeba abiria 101, lakini kwa takwimu zilizopo sasa zinazojumuisha miili iliyopatikana pamoja na manusura, ni wazi kwamba chombo hicho kilikuwa kimebeba abiria kupita kiasi.

Rais Magufuli ameagiza bendera ya taifa ipepee nusu mlingoti.

Ameagiza wote waliohusika na mkasa huo wakamatwe akiwemo kapteni wa kivuko hicho, ambaye taarifa zilizopo, tayari amekamatwa kusaidia katika upelelezi. Kadhalika ameagiza kuundwa kwa timu itakayoshughulika na uchunguzi huo.

Amewataka wanasiasa kutotumia mkasa huu kama 'kiki za kisiasa' na waache vyombo vya dola kufanya kazi yake.

Ad