Home » Nje Ya Afrika » Wabunge Uingereza kujadili mapendekezo ya Waziri Mkuu

Wabunge Uingereza kujadili mapendekezo ya Waziri Mkuu

03 February 2016 | Nje ya Afrika

Wabunge nchini Uingereza wameanza kujadili mapendekezo ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo David Cameron kuhusu mabadiliko ambayo Uingereza inayataka katika Umoja wa Ulaya.

Akiwasilisha mapendekezo yake hivi leo, Cameron amewataka wabunge nchini humo kuunga mkono mapendekezo hayo amabyo yanataka ushiriakiano zaidi na kuangazia ni vipi Uingereza inaweza kunuifaika ndnai ya Umoja huo.

Aidha, Cameron amesema hajawahi kusema kuwa Uingereza haiwezi kufanikwia nje ya Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu huyo pia amesema kuwa, Uingereza inataka ushirkiano zaidi wa kibiashra na usalama sio siasa katika Umoja huo.

Uingereza kuwa na kura ya maoni baadaye mwaka ujao raia wa nchi hiyo kuamua kuendelea kuwa ndani ya Umoja huo au la.
Viongozi wa mataifa kama Ufaransa na ujerumani wamekuwa wakitoa wito kwa Uingereza kuachana na mpango.

Ad