Home » Nje Ya Afrika » Vladimir Poutine ameamua kuahirisha ziara yake jijini Paris

Vladimir Poutine ameamua kuahirisha ziara yake jijini Paris

12 October 2016 | Nje ya Afrika

Rais wa Urusi Vladimir Poutine ameamua kuahirisha ziara yake jijini Paris nchini Ufaransa ambayo ilipangwa kufanyika Octoba 19 ambako alitarajiwa kuzungumza na mwenyeji wake Francois Hollande.

 

Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya Kremlin jijini Moscou Dmitri Peskov, ziara hiyo imeahirishwa kwa sasa, itafanyika pale tu rais wa Ufaransa Francois Hollande atapojiskia vizuri.

 

Hatuwa hii inakuja baada ya rais wa Ufaransa Francois Hollande kuonyesha kusita kukutana na rais Poutine katika kipindi hiki uhusiano wa mataifa haya mawili ukiendelea kudorora kufuatia mzozo wa Syria.

 

Hivi majuzi rais Hollande amesikika akihoji katika kituo kimoja cha televisheni nchini Ufaransa kuhusu umuhimu wa kukutana na rais Poutine katika kipindi hiki nchi yake ikituhumiwa kutekeleza mauaji ya kivita nchini Syria