Home » Nje Ya Afrika » Ugiriki kutumia kidiplomasia kutstua tatizowahamiaji na wakimbizi

Ugiriki kutumia kidiplomasia kutstua tatizowahamiaji na wakimbizi

22 February 2016 | Nje ya Afrika

Serikali ya Ugiriki imesema imeanza juhudi za kidiplomasia kutatua tatizo la maelfu ya wahamiaji na wakimbizi waliozuiliwa katika eneo la mpaka na Macedonia tangu pale nchi hiyo iliponaza kuwazuia wakimbizi kutoka Afghanistan.

Zaidi ya wahamiaji elfu tano wanazuiliwa tangu Jumapili katika eneo la Idomeni mji wa mwisho wa Ugiriki kabla ya kuingia nchini Macedonia ambapo shughuli za zimepungua kuligana na duru za polisi.

Duru wizara ya uhamiaji zinaeleza kuwa wahamiahi na wakimbizi elfu 3 wamewasili Jumatatu mapema asubuhi katika bandari ya Piree, lakini hawakuweza kuruhusiwa kuondoka kuelekea katika mji wa Idomeni.

Waziri anaehusika na uhamiaji Yannis Mouzalas amekimbia kituo cha taifa nchini humo kwamba wameanza juhudi za kidiplomasia na kuna matumaini ya kulipatishai ufumbuzi swala hili.

Kuzuiliwa huko kwa wakimbizi kuingia bara la ulaya ya kati na kaskazini hadi sasa wakimbizi kutoka Syria, iraq na Afghanistan walikuwa wanaruhiswa kuingia kupitia mpaka wa Ugiriki na Macedonia kunakuja baada ya Austria kuchukuwa hatuwa ya kuwapokea waomba hifadhi 80 pekee kwa siku pamoja na kuruhusu wakimbizi 3.200 kutumia mipka yake.

 

Ad