Home » Nje Ya Afrika » Ufaransa ni miongoni mwa mataifa barani Ulaya yaliobeba mzigo wa wakimbizi

Ufaransa ni miongoni mwa mataifa barani Ulaya yaliobeba mzigo wa wakimbizi

20 June 2016 | Nje ya Afrika

Wakati dunia hii leo ikiadhimisha siku ya wakimbizi duniani, nchi ya Ufaransa ni miongoni mwa mataifa barani Ulaya yaliobeba mzigo wa wakimbizi kutoka katika mataifa mbalimbali duniani hususan Syria Eritrea, Sudan na Iraq.

Serikali ya nchi hiyo hivi karibuni ilichukuwa hatuwa za kuuunda kambi za kuwakusanya pamoja wakimbizi hao, lakini hatuwa hii inalaumiwa na wadau wa mwaswala ya wakimbizi ambao wanaona kwamba hakuna umakini katika kuwashughulikia wakimbizi hao na ndio maana muda mfupi hurejea katika maeneo waliokuwa wamepiga kambi kabla ya kupelekwa kambini.