Home » Nje Ya Afrika » Sweden kuwafurusha takriban wahamiaji 80, 000,

Sweden kuwafurusha takriban wahamiaji 80, 000,

28 January 2016 | Nje ya Afrika

Sweden imesema kuwa imedhamiria kuutekeleza mpango wa kuwafurusha takriban wahamiaji 80, 000, na baadaye hatua itafuta maombi yaliyotolewa na wahamiaji kupewa hifadhi nchini humo, wizara ya mambo ya ndani nchini humoi imesema.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Stokholm Waziri wa mambo ya ndani wa Sweden Anders Ygeman amesema mpango huo wa kuwarejesha nyumbani wahamiaji hao utachukua miaka kadhaa.

Ygeman amesema wahamiaji zaidi ya mia moja na sitini elfu walituma maombi ya uhamiaji nchini Sweden mwaka 2015, ikiwa ni idadi ya juu barani Ulaya, na kaongeza kuwa polisi na mamlaka ya uhamiaji wamejipanga kuanzisha mpango huo hivi karibuni.

Sweden inasema hatua ya kuwafurusha wahamiaji hao inakuja baada ya serikali kukadiria kuwa idaidi yao inazidi kuongezeka na kwamba walikuwa wameandika wahamiaji sitini elfu waliofika katika nchi za Scandinavia mwaka jana, lakini cha kushangaza idadi hiyo inazidi kuongezeka.

Pamoja na Ujerumani, mataifa yote ya Scandinavia yameonekana kuwa ni maeneo yanayopendwa sana na wahamiaji wanaoingia barani Ulaya kinyume na sheria.

Ingawa Sweden imesema itafuta maombi ya wahamiaji walitamani kupewa hifadhi nchini Humo, inaarifiwa kuwa imetoa vibali vya kuishi kwa baadhi ya wahamiaji ambao awali walidhihirisha nia ya kuishi nchini humo.

Ad