Home » Nje Ya Afrika » Polisi nchini Indonesia imewakamata zaidi ya watu 30

Polisi nchini Indonesia imewakamata zaidi ya watu 30

15 February 2016 | Nje ya Afrika

Polisi nchini Indonesia imewakamata zaidi ya watu 30 kutoka makundi ya kijihadi wanaoshukiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi nchini humo.

Kukamatwa huko kunakuja baada ya taarifa za kinteljensia kuonesha kuwa, washukiwa hao walikuwa wanapanga kutekeleza mashambulizi ya kigaidi katika uwanja wa ndege katika siku zijazo.

Aidha, polisi wanasema watu hao wamekamatwa baada ya kuanza kwa operesheni ya kuwatafuta magaidi baada ya kutokea kwa shambulizi ya bomu mjini Jakarta na kusababisha vifo vya watu wanne na wenhine kujeruhiwa mwezi uliopita.

Watu 17 miongoni mwa hao 30 wanaelezwa kuhusika moja kwa moja na shambulizi la mwezi uliopita, na wanashukiwa kuwa wanachama wa kundi la Islamic State.

Ripoti zinasema kuwa mmoja wa washukiwa hao Hendro Fernando amewaambia polisi wanaopambana na ugaidi kuwa alipokea Dola 97,000 kutoka kwa serikali ya Jordan, Iarq na Uturuki kutekeleza mashambulizi ya ugaidi katika uwanja wa ndege wa Jakarta na Makao Makuu ya Polisi.

Polisi wanasema, hadi sasa kuna raia wa Indonesia 392 wanaolipigania kundi la Islamic State nchini Syria na wengine 50 wanaaminiwa kuwa na mpango wa kusafiri kwenda Syria kuunda na kundi hilo.

Ad