Home » Nje Ya Afrika » Moise Katumbi alaani polisi cha kuvamia Kanisa la Basilica St Mary jana mjini Lubumbashi

Moise Katumbi alaani polisi cha kuvamia Kanisa la Basilica St Mary jana mjini Lubumbashi

09 March 2016 | Nje ya Afrika

Gavana wa zamani wa mkoa wa Katanga, Moise Katumbi amesema kuwa hakufurahishwa na kitendo cha polisi cha kuvamia Kanisa la Basilica St Mary jana mjini Lubumbashi, wakati alikuwa akishiriki ibada iliyoandaliwa katka muktadha wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

Katumbi alijumuika na wanawake wanachama wa vyama vya upinzani katika muungano wa vyama vya upinzani maarufu kama G7 ambao walikusanyika kusali pamoja katika kuliombea taifa hilo na viongozi wa nchi hiyo,

Imearifiwa kuwa Polisi walifyetua risasi na kuripua mabomu ya kutoa machozi punde baada ya kumalizika kwa ibada, kitendo ambacho Moise Katumbi ameasema ni kinyume na haki za binadamua.

Ad