Home » Nje Ya Afrika » Manuel Valls amekutana na Benjamin Netanyahu

Manuel Valls amekutana na Benjamin Netanyahu

24 May 2016 | Nje ya Afrika

Waziri Mkuu wa Ufaransa Manuel Valls amekutana hapo jana na mwenzake wa Israel Benjamin Netanyahu jijini Yerusalemu kuzungumzia mapendekezo ya kuwepo kwa mkutano wa kimataifa kufufua juhudi za amani na Wapalestina.

Hata hivyo, Netanyahu, ametupilia mbali mapendekezo hayo na badala yake kuomba pawepo na mazungumzo ya ana kwa ana baina yake na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas.

Ad