Home » Nje Ya Afrika » Jeshi la Marekani imeeleza kuwa Kiongozi wa kundi IS Omar le Tchetchen ameuawa

Jeshi la Marekani imeeleza kuwa Kiongozi wa kundi IS Omar le Tchetchen ameuawa

09 March 2016 | Nje ya Afrika

Jeshi la Marekani imeeleza kuwa Kiongozi wa kundi linalojiita Islamic State Omar al-Shishani, maarufu kama Omar le Tchetchen ameuawa katika mashambulizi ya anga yaliotekelezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Taarifa hiyo ya jeshi la Marekani inasema huenda kiongozi huyo ameuawa na wapiganaji wemngine 12 wa kundi hilo katika mashambulio ya anga yaliotumiwa ndege zisizokuwa na rubani pamoja na ndege nyingine za kivita.

Msemaji wa wizara ya ulinzi nchini Marekani Peter Cook amesema, Omar le Tchétchène ambae jina lake halisi ni Tarkhan Tayumurazovich Batirashvili, ni raia wa Georgia lakini baadae alijulikana kama Omar al Shishani na amekuwa katika nyadhifa tofauti za kundi hilo ikiwemo wizara ya kivita.

Kifo chake iwapo kitathibitishwa, kitalidhoofisha sana kundi hilo katika uwezo wake wa kuajiri wapiganaji wa kigeni hususan raia wa Tchetchenia na Kokaze pamoja na kupungua kwa uwezo wake wa kuratibu ngome zake za Raqa na Mossoul nchini Iraq

Mashambulizi hayo yanadaiwa kutekelezwa mwishoni mwa juma lililopita katika eneo la Chadadee, ngome ya wapigajaji wa kijihadi kaskazini magharibi mwa Syria.

Jeshi la Marekani lilikuwa limetowa dola milioni tano kwa mtu yeyote ataetoa taarifa za kukamatwa kwa kiongozi huyo.

Ad