Home » Nje Ya Afrika » Donald Trump rais mpya mteule Marekani

Donald Trump rais mpya mteule Marekani

09 November 2016 | Nje ya Afrika

Donald Trump amemshinda Hillary Clinton katika matokeo ya uchaguzi wa urais uliokuwa na ushindani mkali.

Bi Clinton amempigia simu Bw Trump kumpongeza kwa ushindi wake.

Bw Trump alikuwa ameshinda majimbo mengi muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda.

Alikuwa ameshinda Ohio, Florida, na North Carolina, ingawa Bi Clinton alishinda Virginia.

Kwa sasa Trump ana kura 278 za wajumbe na Clinton 218 kwa mujibu wa makadirio ya RFI. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe.