Home » Nje Ya Afrika » Brazil, zaidi ya raia milioni 3 wameandamana nchi nzima

Brazil, zaidi ya raia milioni 3 wameandamana nchi nzima

14 March 2016 | Nje ya Afrika

Polisi nchini Brazil, inasema kuwa zaidi ya raia milioni 3 wameandamana nchi nzima hapo jana, ikiwa ni maandamano makubwa kuwahi kushuhudiwa nchini humo, wakishinikiza kuondolewa madarakani kwa rais Dilma Rousseff.

Wakiwa wamevalia mavazi ya rangi za njano na kijani kama zilizoko kwenye bendera ya nchi hiyo, wananchi hao wanalenga kuweka shinikizo kwa bunge la Congress nchini humo kuharakisha muswada wa kutokuwa na imani na rais Rousseff wakimlaumu kwa hali ngumu ya maisha na mdororo wa kiuchumi ulioikumba nchi hiyo.

Miongoni mwa viongozi walioshiriki maandamano hayo ni pamoja na wakili, Helio Bicudo aliyekuwa akiiunga mkono Serikali, ambapo sasa anataka wananchi kuweka shinikizo zaidi kwa rais Roussef kuondoka madarakani, akidai kuwa imefika mwisho kwa nchi yao kuporwa na watu wachache.

Ad