Home » Nje Ya Afrika » Aliyeishi muda mrefu na moyo wa kupandikizwa afariki

Aliyeishi muda mrefu na moyo wa kupandikizwa afariki

11 February 2016 | Nje ya Afrika

Bw McCafferty alipatikana na maradhi ya moyo akiwa na umri wa miaka 39.

Alifanyiwa upasuaji na Sir Magdi Yacoub.

Upasuaji wa kwanza wa kupandikiza moyo uliofanikiwa ulifanyiwa nchini Afrika Kusini mwaka 1967 na Prof Christiaan Neethling Barnard na kundi la matabibu 30 katika hospitali ya Groote Schuur, Cape Town.

Mgonjwa wao, Louis Washkansky, alifariki siku 18 baada ya kupokea moyo mpya.

Mwanamume aliyeishi muda mrefu duniani na moyo wa kupandikizwa amefariki, baada ya kuishi miaka 33 na moyo huo.

John McCafferty aliambiwa alikuwa amesalia na miaka mitano pekee ya kuishi alipofanyiwa upasuaji katika hospitali ya Harefield, Middlesex Uingereza mnamo tarehe 20 Oktoba 1982.

Mjane wake Ann amesema: "Miaka 30 iliyopita ilikuwa ya furaha sana. Tulitembea na kujionea ulimwengu.”

Bw McCafferty, kutoka Newport Pagnell eneo la Buckinghamshire, alifariki Jumanne akiwa na umri wa miaka 73 akitibiwa hospitali ya Milton Keynes.

Alitambuliwa na Guiness World Records mwaka 2013 kuwa mtu aliyeishi muda mrefu zaidi na moyo wa kupandikizwa.

Wakati huo alisema: “Ninataka rekodi hii ya dunia iwapo moyo wote wanaosubiri kufanyia upasuaji wa kupandikiza moyo na kwa wale, ambao kama mimi, wamebahatika kupandikizwa moyo mwingine kama mimi.”

 

Ad