Home » Michezo » Leopards washindi kwa mara ya pili kwa kutwaa kombe la CHAN

Leopards washindi kwa mara ya pili kwa kutwaa kombe la CHAN

09 February 2016 | Michezo

Mamia kwa maelfu ya wakaazi wa mji wa Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wamemiminika kwa uwingi kwenye uwanja wa kimataifa wa Ndjili kuwapokea Vijana wa timu ya taifa Leopards washindi kwa mara ya pili kwa kutwaa kombe la CHAN mjini kigali nchini Rwanda kwa kuifunga Timu ya Mali mabao matatu-bila.

Spika wa bunge la kitaifa nchini DRC Aubin Minaku ndiye amewapokea wachezaji hao wakiwa na kombe hilo wakati mamia kwa maelfu ya mashabiki wakiwa wamejipanga kwenye barabara Patrice Emery Lumbumba.
Hayo yanajiri wakati hapo jana Polisi mjini humo walilazimika kuwavuru mishia bomu za kutoa machozi maelfu ya mashabiki wa timu hiyo, wakati walipokuwa wakisherehekea ushindi wa timu ya nchi yao .

Mashuhuda wanasema mashabiki hao walikuwa wakiimba nyimbo zinazo mkashifu rais Joseph Kabila, nao walitawanyika katika barabara mbalimbali huku polisi ikizidisha ulinzi katika barabara kuu.

Ad