Home » Makala » Parachichi la Tanzania kinara katika soko la kimataifa

Parachichi la Tanzania kinara katika soko la kimataifa

29 January 2018 | Makala

Soko kubwa na bei Nzuri ya Parachichi la Tanzania imeimarika Nchi za Ulaya  za Denmark, Ufaransa, Uholanzi, Norway, Hispania na Uingereza Likitoa fulsa mpya ya Ustawi wa  zao hili kwa Watanzania, imebainika  kwamba Parachichi ya Tanzania imechukua chati ya Ubora katika Soko hilo.

 
Uchunguzi kitakwimu una baini Mwaka 2012, kiasi cha mauzo ya nje ya Parachichi la Tanzania yalikuwa kilo 488,492 tu, Miaka mitatu baadae Mwaka 2015 Tanzania ilisafirisha Kilo 2,579,976 Ikiwa ni ongezeko la 428.48%.
 
Kwa mujibu wa Kampuni ya Africado ambayo ni  kampuni ya kwanza ya Tanzania inayosafirisha Parachichi la Tanzania nchini Uingereza ambako maduka makubwa vyakula ya Ocado, Sainsbury, Tesco na Waitrose, Parachichi ya Tanzania inatajwa kuwa Bora zaidi katika soko hilo la Ulaya.
 
Walaji wa Ulaya wamenogewa na Parachichi la Tanzania linalo zalishwa Mufindi na Kilolo likitajwa kupatikana msimu ambao Nchi zaidi ya Kumi zinazozalisha Tunda hili kuwa Nje ya Msimu wa Uvunaji wa Zao hili
Parachichi linazaliswa na Nchi zaidi ya 10 Duniani  zikiwemo Argentina, Brazil, Chile, Colombia, Dominican Republic, Israel, Kenya, Mexico, Morocco, Peru, South Africa, Spain, Swaziland, Tanzania
 
Zao la Parachichi la Tanzania limeonyesha mwenendo mzuri wa bei na Soko kubwa Ulaya likiuzwa kwa hadi Sh za Kitanzania 7000 ama Paun 1.95 hii leo,fulsa hii inaangukia Tanzania
 
Kipindi cha mavuno cha sasa ni Juni hadi Agosti, Huku Tanzania pekee inaweza kuvuna na kusambaza kuanzia mwezi Machi hadi Oktoba
 
Sisi Kama Taifa ni Muda sasa wa kuacha mambo yasiyo ya Msingi na kujikita na Fursa kubwa ya kilimo cha Parachichi la Tanzania,Tumeona MatokeoChanyA+ katika Korosho na Sasa Taifa Turudi kujikita na kilimo na hasa kunapojitokeza fulsa mazao kama Parachichi.
 
 
 
 
 
Ad