Home » Makala » MAGUFULI aahidi kuhubiri amani

MAGUFULI aahidi kuhubiri amani

16 November 2015 | Makala

Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi -CCM Dakta JOHN MAGUFULI amesema kuwa siku zote katika maisha yake atahubiri amani kwa watanzania vinginevyo hafai kuwa Rais kwa kuwa amani ndio msingi wa maendeleo ya taifa lolote duniani.

Dakta MAGUFULI amesema hayo Mjini BUTIAMA katika mkutano wake wa kwanza wa Kampeni  Mkoani MARA.

Dakta MAGUFULI amesema mara baada ya kupata ridhaa ya kuongoza nchi Mkoa wa MARA utakuwa na umeme wa uhakika ikiwa ni muendelezo wa jitihada za Serikali ya Awamu ya Nne kwa kuvuka lengo la Ilani ya CCM ya mwaka 2010/15 kwa kusambaza umeme nchi nzima kutoka Asilimia 30 zilizokusudiwa hadi Asilimia zaidi ya 40