Home » Makala » BAWACHA ZANZIBAR kushusha bendera

BAWACHA ZANZIBAR kushusha bendera

16 November 2015 | Makala

Baraza la  Wanawake  CHADEMA  BAWACHA  ZANZIBAR  limepanga  kushusha  bendera zote  za CHADEMA  Kisiwani  Zanzibar  ndani  ya masaa 24  endapo  ombi lao la kurejesha viti vyao maalum  katika mikoa mitano  Unguja na Pemba  halitazingatiwa.

Akitoa taarifa hiyo mjini  Unguja mbele ya vyombo vya habari   Makamu  Mwenyekiti wa BAWACHA  ZANZIBAR Bibi HAMIDA ABDALLAH  HUWEISHI  amesema wakiwa kama wanachama hai wa CHADEMA hawaoni sababu ya Baraza kuu la CHADEMA kudharau ombi hilo kutokana na Baraza hilo la CHADEMA  la Wanawake  limeweza kufanya kazi kubwa Zanzibar  ili kuhakikisha  ushindi mkubwa wa Mheshimiwa LOWASSA  kupatikana.

Hivi  karibuni  Kaimu Katibu  Mkuu wa CHADEMA SALUM MWALIMU  alitangaza majina ya wabunge wawili wateule wa viti maalum  kutoka katika Mikoa miwili  tu ikiwa ni  Unguja na Pemba  jambo ambalo BAWACHA Zanzibar  hawakuweza kukubaliana  nalo