Home » Burudani » Koffi Olomide amekamatwa jijini Kinshasa

Koffi Olomide amekamatwa jijini Kinshasa

26 July 2016 | Burudani

Mwanamuziki maarufu kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Koffi Olomide amekamatwa jijini Kinshasa kwa kosa la kumpiga teke mnenguaji wake wa kike jijini Nairobi nchini Kenya mwishoni mwa juma lililopita.

Masaibu ya Olomide yameendelea kushuhudiwa kwa juma la pili baada ya kukamatwa na kufukuzwa nchini Kenya kutokana na tukio hilo.

Waandalizi wa tamasha lingine nchini Zambia hapo jana walitangaza pia kusitisha tamasha la mwanamuziki huyu baada ya tukio hilo.

Polisi nchini DRC wanasema mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 60 anashikiliwa kwa mohojiano zaidi kutokana na tukio la Nairobi.