Home » Bunge » Serikali yasikitishwa watanzania kudhalilishwa India

Serikali yasikitishwa watanzania kudhalilishwa India

05 February 2016 | Bunge

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi AUGUSTINE MAHIGA amesema serikali ya TANZANIA imesikitishwa na taarifa za wanafunzi wanne raia wa TANZANIA wanaosoma nchini INDIA kudhalilishwa hivi karibuni wakiwa nchini humo.

 

Akitoa taarifa ya serikali bungeni mjini DODOMA, Waziri MAHIGA amesema serikali imepokea taarifa za wanafunzi hao walio dhalilishwa na kuumizwa kutokana na fujo za kibaguzi zilizotokea BANGALORE nchini INDIA na kumwagiza Balozi wa TANZANIA nchini INDIA kufuatilia suala hilo.

 

Amesema serikali ya TANZANIA ingependa kuona hatua za kisheria zikichukuliwa dhidi ya watu waliohusika na vitendo hivyo.

 

Fujo hizo zinaelezwa kutokea siku ya Jumanne wiki hii baada ya mwanafunzi anayesoma nchini INDIA raia wa SUDAN kumgonga mwanafunzi wa INDIA.