Home » Bunge » Rais Dkt. John Pombe Magufuli apokea Hundi Kifani kutoka kwa Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson

Rais Dkt. John Pombe Magufuli apokea Hundi Kifani kutoka kwa Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson

12 April 2016 | Bunge

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kulia, Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah pamoja na wafanyakazi wengine wa Bunge wakiwa wameishika hundi Kifani hiyo yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita. Rais Dkt. Magufuli ameipongeza Taasisi ya Bunge kutokana na hatua hiyo ya kubana matumizi na kuamua fedha zao zitumike katika kununulia madawati kwa ajili ya wanafunzi.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson kabla ya kukabidhiwa hundi kifani yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sita.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika tukio hilo la upokeaji wa Taarifa yaUtendaji wa TAKUKURU pamoja na upokeaji wa Hundi Kifani kutoka Taasisi ya Bunge Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John Kijazi wapili kulia, Dkt. Tulia Ackson wakwaza kulia, Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashilillah wakwanza kushoto, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna Valentino Mlowola Ikulu Jijini Dar es Salaam.