Home » Biashara » SERIKALI KUPATA MABILIONI YA SHILINGI KUTOKANA NA ALMASI ILIYOKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA JNIA

SERIKALI KUPATA MABILIONI YA SHILINGI KUTOKANA NA ALMASI ILIYOKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA JNIA

09 November 2017 | Biashara

 

Waziri wa Madini, Angela Kairuki amesema kuwa serikali inataraji kupata mrabaha zaidi katika madini ya Almasi yaliyokamatwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere kutoka kwa Kampuni ya Williamson Diamond iliyokuwa ikitaka kutoroshwa madini nchini kwenda Ubelgiji.

Waziri Kairuki amesema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari wakati akitoa ripoti ya Wizara ya Madini juu ya mzigo huo wa Almasi kutoka kampuni ya Williamson Diamonds.
“tarehe 20/10/2017 almasi hizo zilisafirishwa kwenda ubelgiji na serikali ilituma maafisa wake kusimamia uuzwaji wa alamasi hizo ambapo tarehe 7/11/2017 almasi hizo ziliuzwa kwa dola za Marekani 10,261,227.76 hivyo thamani hii ni ongezeko la Dola za Marekani 2,069,582.77 sawa na asilimia 20.16%”amesema.

Amesema kutokana na ongezeko hilo baada ya almas kuuzwa serikali itapata mrabaha zaidi ambao ni mwisho kiasi cha Dola za Marekani 124,174,.97 na ada ya ukaguzi Dola za marekani 20,695.83 ambayo jumla yake ni dola za Marekani 144,870.80 sawa na shilingi Milioni 325.525 hivyo jumla ya mapato yote ya serikali kutokana na mauzo ya almasi hizi ni Dola za Marekani 718,288.95

Aidha Waziri Kairuki amesema katika mzigo huo waliweza kuikuta Almasi moja yenye rangi ya pinki ambayo ni adimu kupatikana na yenye uzito wa karatani 5.92 na kuuzwa kwa dola za marekani 2,005,555.00 sawa na shilingi Bilioni 4.51.

Alimaliza kwa kusema kuwa anawakikishia Watanzania kuwa serikali itaendelea kuisimamia kwa makini rasilimali zetu za madini ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inanufaika ipasavyo.

Waziri wa Madini, Angela Kairuki akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya ripoti ya faida iliyopata serikali katika Madini ya Almas kutoka mgodi wa Wiliamson Diamonds Ltd iliyokamatwa uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila akitoa ufafanuzi wa kitaalmu juu ya madini hayo yaliyouzwa huko ubelgiji.Kamishana wa Madini, Mhandisi Benjamini Mchwampaka akizungumzia juu ya madini hayo yanavyoweza kuliongezea pato taifa.

Ad