Home » Afrika

Afrika

12 May 2016
RAIS Yoweri Museveni leo ametawazwa rasmi kuwa Rais mpya wa Uganda kwa muhula wa tano mfululizo.Tayari Rais Museveni amekwisha tawala miaka 30. Kutawazwa kwake leo, ambako kunashuhudiwa na viongozi wa mataifa 14 kutoka Afrika na wageni wengine mashuhuri, kuna fuata ushindi uliojaa ubishani katika uchaguzi wa Februari 18.
06 May 2016
Mfanyabiashara mashuhuri nchini Kenya Jacob Juma, ambaye amekuwa akizua mjadala mitandaoni kutokana na ujumbe wake anaoandika hasa kwenye Twitter, ameuawa kwa kupigwa risasi jijini Nairobi. Taarifa zinasema Juma alipigwa risasi na watu ambao walikuwa wakiendesha pikipiki alipokuwa akielekea nyumbani kwake mtaa wa Karen majira ya saa nne usiku hapo... [Read More]
06 May 2016
Kikosi cha jeshi la Uganda la UPDF kinachohudumu nchini Somalia hakijapata mishahara yake ya miezi minne huku wabunge wa nchi hiyo wakitaka jeshi hilo kuondolewa nchini humo,
06 May 2016
Shutuma kuhusu shambulizi baya la anga kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao kaskazini mwa Syria zimeongezeka leo Ijumaa wakati serikali ikikanusha kuhusika, wakati huohuo mpango tete wa kusitisha mapigano ukitekelezwa katika uwanja wa vita mjini Aleppo. Wanawake na watoto wameripotiwa kuwa miongoni mwa raia 28 waliouawa katika mashambulizi... [Read More]
05 May 2016
Baada ya siku sita kufunikwa na vifusi vya jengo la makaazi ya orofa saba liliporomoka katika mtaa wa Huruma jijini Nairobi nchini Kenya, mwanamke mja mzito ameokolewa akiwa hai. Maafisa wa uokoaji wanasema yuko hospitalini anakoendelea kupata matibabu pamoja na kwamba hakuumia hata kidogo. Mapema wiki hii, mtoto wa mwaka mmoja pia aliokolewa... [Read More]
05 May 2016
Hali ya utulivu imeshuhudiwa leo katika mji wa Allepo nchini Syria baada ya Marekani na Urusi kufikia mwafaka wa kusitisha mapigano ambao yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya wiki mbili na kusababisha mamia ya watu kupoteza maisha. Jeshi la Syria limesema litatii mkataba huo ambao unatarajiwa kushuhudiwa kwa siku mbili zijazo. Rais Bashar Al Assad... [Read More]
05 May 2016
Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC inasema haijiuzulu licha ya kuendelea kupata shinikizo kutoka kwa wanasiasa wa upinzani kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka ujao. Makamishena wa Tume hiyo wanasema, wao sio mafisadi na wala hawaegemei upande mmoja kama inavyodaiwa na muungano wa CORD. Mwenyekiti wa Tume hiyo Isaak Hassan akizungumza leo na wanahabari... [Read More]
05 May 2016
Serikali ya Zimbabwe inapanga kuchapisha noti zake za kifedha zinazofanana na Dola ya Marekani kukabiliana na uhaba wa fedha nchini humo. Gavana wa Benki Kuu nchini humo John Mangudya amesema mpango huo utaungwa mkono na Benki ya uingizaji na upokeaji kwa kima cha Dola za Marekani 200. Aidha ameeleza kuwa kutakuwa na sarafu na noti ya Dola, 2, 5... [Read More]
05 May 2016
Serikali ya Uganda imepiga marufuku vyombo vya Habari nchini humo kupeperusha matangazo ya moja kwa moja maandamano ya upinzani yakiongozwa na Kizza Besigye kutoka chama cha FDC kuendelea kupinga ushindi wa rais Museveni mwezi Februari. Hii inamaanisha kuwa vyombo vya Habari haviruhusiwi kuwahoji wanasiasa wa upinzani au kuonesha shughuli zao za... [Read More]
05 May 2016
Siku moja baada ya Gavana wa zamani wa Jimbo la Katanga nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Moise Katumbi Chapwe kutangaza nia yake ya kuwania urais mwezi Novemba kupitia muungano wa vyma vya upinzani, serikali nchini humo imeamuru uchunguzi kufanyika dhidi ya mwanasiasa huyo kutumia mamluki kutoka Marekani kumlinda. Hata hivyo, madai haya... [Read More]

Pages

Subscribe to Afrika