Home » Afrika » Viongozi wa upinzani nchini Kenya wakiongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga,

Viongozi wa upinzani nchini Kenya wakiongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga,

16 June 2016 | Afrika

Viongozi wa upinzani nchini Kenya wakiongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, wamezuiliwa na polisi kuonana na wanasiasa sita wa upinzani na serikali wanaozuiliwa katika kituo cha polisi cha Pangani jijini Nairobi kwa madai ya kutoa matamshi ya uchochezi.

Viongozi hao wameshtumu hatua ya serikali kuwazuia wanasiasa hao kwa siku ya tatu leo bila ya kuwafungulia mashtaka na kukata wapendwa wao kuonana nao.Inaripotiwa kuwa wanasiasa hao wamekataa kula chakula cha rumande na wapendwa wao waliowapelea chakuka la nguo za kubadilisha walizuiliwa.Upinzani sasa unataka wanasiasa wote kuachiliwa huru kwa saa 24 zijazo la sivyo watachukua hatua.

Mahakama siku ya Jumanne iliamuru wanasiasa hao kuzuiliwa hadi kesho ili kuruhusu polisi kukamilisha uchunguzi dhidi yao. Moses Wetangula ni mmoja wa muungano wa upinzani CORD.

Ad