Home » Afrika » Upinzani nchini Congo Brazaville umeendelea kusisitiza kuwa hautambui matokeo ya rais

Upinzani nchini Congo Brazaville umeendelea kusisitiza kuwa hautambui matokeo ya rais

25 March 2016 | Afrika

Upinzani nchini Congo Brazaville umeendelea kusisitiza kuwa hautambui matokeo ya rais yaliyotangazwa juma hili na tume ya uchaguzi nchini humo ambapo yamempa ushindi wa kishindo rais wa sasa Denis Sassou Nguesso.

 Kiongozi wa upinzani nchini humo, Guy-Brice Parfait Kolelas amesema kuwa, matokeo hayo ni yakutengenezwa na kwamba uchaguzi ulifanyika katika mazingira ya usiri mkubwa hali iliyoashiria waziwazi kuwa huenda kuna njama za kupanga matokeo.

 

Guy-Brice Parfait Kolelas anasisitiza kuwa matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu yamekuwa ni kichekesho.

Ad