Home » Afrika » Ufaransa na Misri zitaajiri kampuni mbili binafsi kusaidia katika utafutaji wa visanduku nyeusi

Ufaransa na Misri zitaajiri kampuni mbili binafsi kusaidia katika utafutaji wa visanduku nyeusi

27 May 2016 | Afrika

Ufaransa na Misri zitaajiri kampuni mbili binafsi kusaidia katika utafutaji wa visanduku nyeusi vya ndege ya Misri MS 804 iliyoanguka baharini juma lililopita wakati ikitoka Paris kwenda Cairo, Wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa imesema.

Msemaji wa wizara hiyo amesema wako katika mazungumzo na kampuni mbili binafsi kwa kushirikiana na serikali ya Misri,na kuongeza kuwa lengo ni kuhamasisha vyanzo vya kuwezesha zoezi hilo kwa haraka zaidi.

Duru za kidiplomasia mjini Paris zinasema makampuni hayo mawili, yote ya Kifaransa, ni (DOS) na Alseamar, yenye makao makuu yake jijini Paris Ufaransa.

Ad