Home » Afrika » Serikali ya Zimbabwe kuchapisha noti zake zinazofanana na Dola ya Marekani

Serikali ya Zimbabwe kuchapisha noti zake zinazofanana na Dola ya Marekani

05 May 2016 | Afrika

Serikali ya Zimbabwe inapanga kuchapisha noti zake za kifedha zinazofanana na Dola ya Marekani kukabiliana na uhaba wa fedha nchini humo.

Gavana wa Benki Kuu nchini humo John Mangudya amesema mpango huo utaungwa mkono na Benki ya uingizaji na upokeaji kwa kima cha Dola za Marekani 200.

Aidha ameeleza kuwa kutakuwa na sarafu na noti ya Dola, 2, 5 10 na 20 na zitakuwa na thamani sawa na zile za Marekani.

Nchi ya Zimbabwe imekuwa ikabiliwa na changamoto za kifedha hasa baada ya kushuka thamani kwa sarafu yake kuanzia mwaka 2009 na kuamua kuanza kutumia Dola ya Marekani.

Tangu kipindi hicho, pamoja na Dola raia wa Zimbabwe wamekuwa wakitumia sarafu ya Rand ya Afrika Kusini na Yuan ya China katika shughuli za ununuzi na maswala mengine muhimu.

Kwa sasa viongozi wa Benki, wanaendelea kujadiliana kuhusu mwonekano wa noti hiyo na uamuzi utataolewa baada ya miezi miwili ijayo.

 

Ad