Home » Afrika » Rais wa zamani wa Burkina Faso amepewa uraia Cote D'Ivoire

Rais wa zamani wa Burkina Faso amepewa uraia Cote D'Ivoire

24 February 2016 | Afrika

Rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaore amepewa uraia wa nchi ya Cote D'Ivoire baada ya maombi yake kukubaliwa na serikali ya nchi hiyo kufuatia kukimbia nchini mwake mwezi Oktoba 2014.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya taifa, Blaise Compaore pamoja na mdogo wake aliyetajwa kwa jina la Francois wamepewa uraia wa taifa hilo baada ya hatua hiyo kuwa imetangazwa katika katika gazeti la serikali mwezi uliopita.

Gazeti hilo mla serikali limeonyesha kuwa tamko la kupewa uraia lilisainiwa na rais wa Cote D'Ivoire Alassane Ouattara Novemba 17 mwaka 2014 siku chache baada ya Compaore kukimbili nchini humo kufuatia machafuko yaliyosababishwa kukoma kwa utawala wake wa miaka 27 nchini Burkina Faso.

Compaore anatafutwa na Serikali ya Burkina Faso kwa tuhuma za kuhatarisha usalama huku waranti wa kimataifa wa kukamatwa kwake ukiwa umetolewa ukimhusisha na mauaji rais wa zamani wa nchi hiyo Thomas Sankara.

Ad