Home » Afrika » Rais wa Syria amemhakikishia rais wa Urusi kuheshimu makubaliano

Rais wa Syria amemhakikishia rais wa Urusi kuheshimu makubaliano

24 February 2016 | Afrika

Rais wa Syria Bashar al-Assad amemhakikishia rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu utayari wake wa kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa na Marekani na Urusi .

Rais wa Bashar al-Assad ametoa hakikisho hilo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na rais Vladimir Putin na kukubaliana kuwa makubaliano hayo ni mwongozo muhimu katika kufikia mwafaka wa mgogoro wa Syria.

Hatua hiyo imekuja muda mchache baada ya kuwepo wasiwasi wa utekelezwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa na Marekani na Urusi.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya Urusi imesisitiza kuwa rais wa Syria Bashar al-Assad amethibitisha utayari wa serikali yake kuwezesha utekelezaji wa makubaliano hayo ambayo hayahusi makundi mengine ya kijihadi kama vile Islamic State.

Ad