Home » Afrika » Rais Dkt. Magufuli azindua rasmi daraja la Kimataifa la Rusumo Nchini Rwanda

Rais Dkt. Magufuli azindua rasmi daraja la Kimataifa la Rusumo Nchini Rwanda

06 April 2016 | Afrika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Aprili 6, 2016 amezindua daraja la kimataifa la Rusumo na Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha
Rusumo.  

 

Zoezi hili la uzinduzi  limefanyika kwa pamoja kwa husisha  Rais Mhe. Dkt. Magufuli wa Tanzania na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, pia tukio hili limehudhuriwa na viongozi wa ngazi za
juu serkalini kutoka Nchi zote mbili, Mabalozi, na Viongozi wa Taasisi mbambali za Kitaifa na Kimataifa.

Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma kwa Pamoja Mpakani ni kiungo muhimu katika Ukanda wa Kati(Central Corridor), mtandao huu wa barabara unaunganisha barabara kuu ya
Dar es Salaam –  Chalinze – Morogoro – Dodoma – Singida – Nzega – Tinde – Isaka – Lusahanga na Rusumo kupitia Kibingo Nakayonza hadi Kigali Nchini Rwanda. Mtandao huu utakuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kati ya Nchi hizi mbili za Tanzania na Rwanda.


Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa mradi huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Magufuli aliwahimiza Wananchi wa Nchi zote mbili kutumia fursa ya uwepo wa
Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma kwa Pamoja Mpakani Rusumo kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Jumuiya yetu Afrika Mashariki kwa ujumla. 

Aidha Mhe. Rais amewaasa Wananchi kulinda miundombinu kwani kuna baadhi
ya wananchi wanadiriki kuiba alama za barabarani, vyuma vya madaraja na
kuharibu taa za barabarani kwa baadhi ya miji, ameagiza vyombo vya usalama
kuhakikisha wanalinda miundombinu hiyo na kuwachukulia hatua za kisheria kwa
wale watakaodiriki kufanya uharibifu huo.


Aidha licha ya mradi huo kurahisha usafairishaji wa bidhaa na watu Kwa upande wake Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa alieleza faida kadhaa za mradi huo zikiwemo; kuwa ni kiungo muhimu cha kuiunganisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya nyingine za Kikanda kama vile  SADC na COMESA, kurahisisha mawasiliano ya kijamii baina ya watu wa Tanzania na Rwanda, pamoja na kuimarisha uhusiano na kukuza biashara kati ya Nchi hizi mbili za Tanzania na Rwanda na Nchi nyingine za Maziwa Makuu.


Ujenzi wa Daraja la Kimataifa la Rusumo na Kituo cha huduma Pamoja Mpakani Rusumo ni moja ya  miradi inayotekelezwa kwa msaada kutoka Serikali ya Japan kwa Nchi za Tanzania na Rwanda kupitia shirika lake la maendeleo la JICA.

Mradi huu kwa upande wa Tanzania umegharimu takribani kiasi cha TShs. 33,206,508,072.07 hadi kukamilika. Miradi mingine inayotekelezwa kwa kushirikiana
na Serikali ya Japan kupitia JICA ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya Arusha – Namanga, Iringa – Dodoma, Namtumbo – Kilimasera – Matemanga – Tunduru pamoja na barabara ya Masasi – Mangaka.

Ad