Home » Afrika » NRM kwa mara nyingine kimejizolea wingi wa viti Bungeni

NRM kwa mara nyingine kimejizolea wingi wa viti Bungeni

24 February 2016 | Afrika

Chama tawala nchini Uganda cha Rais Yoweri Kaguta Museveni, NRM kwa mara nyingine kimejizolea wingi wa viti Bungeni katika uchaguzi wa Rais na Wabunge uliofanyika juma lililopita nchini humo.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi yanayoendelea kutolewa na Tume ya Uchaguzi ya Uganda cha NRM kinatarajiwa kuchukua viti 427 vya ubunge wakati matokeo ya mwisho yatakapokuwa yametollewa wiki ijayo.

Hata hivyo katika uchaguzi huo uliomrejesha Rais Yoweri Museveni madarakani katika muhula wa tano, Mawaziri 17 wa Chama cha NRM wameshindwa kutetea viti vyao vya Ubunge akiwemo waziri wa ulinzi Crispus Kiyonga anayeongoza jitihada za kikanda za kusaka amani nchini Burundi.

Ad