Home » Afrika » Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Uganda, kuhojiwa na mawakili wa Amama Mbabazi

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Uganda, kuhojiwa na mawakili wa Amama Mbabazi

14 March 2016 | Afrika

Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi nhini Uganda, Badru Kigundu, hii leo anatarajiwa kuhojiwa na mawakili wa upande wa Amama Mbabazi kwenye kesi ya kupinga matokeo ya urais yaliyomrejesha madarakani rais Yoweri Kaguta Museveni.

Mawakili wa Mbabazi walimwandikia barua msajili wa mahakama ya juu nchini humo, kumuarifu kuwa wakati kesi hii inapoanza hivi leo, wanataka kumuhoji mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi, Badru Kigundu kama shahidi wa kwanza kwenye kesi hiyo.

Ikiwa mahakama itakubaliana na ombi la mawakili wa Mbabazi, basi mwenyekiti huyo wa tume anatarajiwa kuopanda kizimbani baade hii leo ama keshp, ambapo kulingana na ratiba ya kesi hiyo, mawakili wa Mbabazi wanazo siku mbili za kuwaslisha kesi yao.

Ad