Home » Afrika » Miili ya wahamiaji 34 ilitupwa na walanguzi wa biashara haramu ya binadamu imepatikana

Miili ya wahamiaji 34 ilitupwa na walanguzi wa biashara haramu ya binadamu imepatikana

16 June 2016 | Afrika

Miili ya wahamiaji 34 ikiwemo ya watoto 20, ambayo ilitupwa na walanguzi wa biashara haramu ya binadamu imepatikana katika Jangwa moja nchini Niger.

Ripoti zinasema kabla ya watu hao kupoteza maisha walikuwa safarini kwenda kutafuta hifadhi katika nchi jirani ya Algeria.

Kupatikana kwa miiili ya watu hao kumethibitishwa na Wizara ya Mambo ya ndani nchini Niger.

Inaelezwa kuwa huenda watu hao waliangamia kwa ukosefu wa maji ya kunywa na ukosefu wa chakula kutokana na joto jingi katika eneo la Assamaka katika jangwa hilo kati ya Niger na Algeria.

Hadi sasa ni miili ya watu wawli tu ndio iliyotabuliwa, mwanaume na mwanamke mwenye umri wa miaka 26 wote kutoka Niger, na inaonekana kuwa waliachwa na walanguzi hao baada ya hali kuwa mbaya.

Maelfu ya wahamiaji haramu wamekuwa wakiwasili nchini Algeria katika siku za hivi karibuni hasa kutoka Mali na Niger kwa sababu ya ugumu wa maisha, wengi wakiwa na malengo ya kupitia nchini humo kwenda barani Ulaya.

Ad