Home » Afrika » Hatimaye Umoja wa Mataifa umeunga mkono juhudi za Kenya

Hatimaye Umoja wa Mataifa umeunga mkono juhudi za Kenya

16 June 2016 | Afrika

Hatimaye Umoja wa Mataifa umeunga mkono juhudi za Kenya za kuwarudisha maelfu ya wakimbizi raia wa Somalia nchini mwao na kufungwa kwa kambi ya wakimbi ya Dadaab.

Uamuzi huu umekuja baada ya rais Uhuru Kenyatta kukutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, jinini Brussels nchini Ubelgiji.

Kenya imekuwa ikisema itawarudisha nyumbani wakimbizi hao na kuhakikisha kuwa wanaondoka kwa usalama, ikisema sababu yake kuu ni ya kiusalama.

Moon amesema, Umoja wa Mataifa utatafuta fedha ili kuisaidia Kenya kuwarudisha nyumbani wakimbizi hao kwa njia nzuri na ya kibinadamu.

 

Ad