Home » Afrika » Hali ya utulivu imeshuhudiwa leo katika mji wa Allepo nchini Syria

Hali ya utulivu imeshuhudiwa leo katika mji wa Allepo nchini Syria

05 May 2016 | Afrika

Hali ya utulivu imeshuhudiwa leo katika mji wa Allepo nchini Syria baada ya Marekani na Urusi kufikia mwafaka wa kusitisha mapigano ambao yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya wiki mbili na kusababisha mamia ya watu kupoteza maisha.

Jeshi la Syria limesema litatii mkataba huo ambao unatarajiwa kushuhudiwa kwa siku mbili zijazo.

Rais Bashar Al Assad hata hivyo amesema hatakubali wanajeshi wake kushindwa katika mji huo uliopo Kaskazini mwa nchi hiyo.

Waangalizi wa maswala ya Haki za Binadamu wanasema wakaazi wa mji huo wameonekana wakiendelea na shughuli zao za kawaida na hakujashuhudiwa mashambulizi yoyote ya angaa.

Ad