Home » Afrika » Francois: jitihada za ziada zinahitajika kuharakisha kusaka ufumbuzi libya.

Francois: jitihada za ziada zinahitajika kuharakisha kusaka ufumbuzi libya.

09 March 2016 | Afrika

Jeshi la Tunisia limewekwa katika hali ya tahadhari baada ya kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi katika mji wa Ben Guerdan ulioko karibu na mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Libya ambapo iliarifiwa kuwa Watu 53 waliuawa.

Kuliripotiwa na mapigano makali juzi jumatatu kati ya jeshi la serikali ya Tunisia na wapiganaji wa kijihadi hali ambayo imewapelekea maafisa wa jeshi la serikali ya Tunis kutangaza marufuku ya kutotoka nje na kuwataka wakaazi wa mji huo wa Ben Guerdan wabaki majumbani mwao.

Kufwatia hali hiyo ya mashambulizi ya kigaidi, rais wa Ufaransa Francois hollande yeye anaona kuwa jitihada za ziada zinahitajika kuharakisha juhudi za kusaka ufumbuzi wa mzozo wa libya.

Ad