Home » Afrika » Andre kimbuta ameruhusu maandamano

Andre kimbuta ameruhusu maandamano

25 May 2016 | Afrika

Gavana wa Kinshasa nchini DRC Andre kimbuta ameruhusu maandamano ya upinzani yaliyopangwa kufanyika kesho siku ya Alhamisi, Mei 26 jijini humo kufuatia mkutano na ujumbe wa jukwaa la upinzani unaotarajiwa kutolewa ikiwa ni pamoja na kupinga hukumu ya Mahakama ya Katiba ambayo inamruhusu Rais Kabila kubaki madarakani ikiwa uchaguzi wa rais utahairishwa.

Baada ya mkutano wa hapo jana uliodumu kwa takriban saa mbili baina ya Gavana huyo na viongozi wa Upinzani kwa ushiriki wa maafisa wa polisi na MONUSCO mratibu wa maandamano hayo ya upinzani Albert Fabrice Puela ametoa wito kwa wananchi wa DRC kuhamasika kwa ajili ya maandamano hayo ambayo yamepigwa marufuku katika baadhi ya miji nchini humo ikiwa ni pamoja na Lubumbashi na Kasai oriental.

Ad